Thursday, October 17, 2019



Mwanariadha, Eliud Kipchoge, ambaye anasherehekewa zaidi nchini Kenya na kote duniani kwa kuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya masaa mbili, alirejea nchini Kenya kimya kimya siku ya jana bila mbwembwe na bila mapokezi yoyote.

Mnamo Oktoba 12 mwaka huu Kipchoge alikuwa mtu wa kwanza kukimbia umbali wa kilomita 42 kwa saa moja, dakika 59 na sekunde 40 katika mashindano maarufu INEOS 1:59 challenge,iliyofadhiliwa na bilionea wa Uingereza Jim Ratcliffe, mmiliki wa kampuni kubwa ya kemikali ya INEOS.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika Shirika la Kenya Airways, Dennis Kashero amesema Kipchoge aliwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA saa kumi na mbili mapema leo, baada ya kusafiri kwa ndege ya KQ117 kutoka Amsterdam.

Kuwasili kwake kulikuwa na tofauti kubwa na alivyoondoka kuelekea Vienna, Austria wakati INEOS ilipotuma ndege ya kibinafsi.

Mwanariadha huyo alirejea nyumbani kimya kimya baada ya kuuzuzua ulimwengu kwa kuwa mtu wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa chini ya masaa mawili,licha ya raia kuwa na matarajio makubwa ya kumpokea.

0 comments:

Post a Comment