Thursday, October 17, 2019



Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Kun Aguero jana Jumatano asubuhi alipata ajali ya gari wakati akielekea katika uwanja wa mazoezi wa timu yake huko jijini Manchester.

Aguero akiwa katika jiji la Manchester njiani kuelekea mazoezini alipata ajali hiyo akiwa na gari lake binafsi aina ya Range Rover linaloweza kufikia thamani ya pauni 150,000 (Tsh milioni 400).
Chanzo cha ajali hakijawekwa wazi.

Katika ajali hiyo mchezaji huyo hakuumia wala kupata jeraha lolote zaidi ya gari kuharibika.

Aguero alikuwa anaenda katika viwanja vya mazoezi vya Man City lakini anaripotiwa kuwa hakuwa anaenda kufanya mazoezi.

Hii ni mara ya pili kupata ajali tangu ajiunge na City mwaka 2011, mara ya kwanza alipata ajali mwaka 2017 Amsterdam Holland baada ya taxi aliyokuwa amepanda kuelekea uwanja wa ndege kwenda kugonga nguzo ya taa za barabarani na kusababisha akaumia katika mbavu.

Muargentina huyo hakuenda kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa kutokana na kutokuwa fiti ,na kocha wa Argentina Lionel Scaloni wiki hii amesema kuwa anataraji kumuita katika kipindi kijacho cha mechi za kimataifa.

0 comments:

Post a Comment