Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije huenda akawa na wakati mgumu kutokana na aina ya matokeo ambayo timu hiyo imekuwa ikipata tangu aanza kuinoa kwa kushindwa kupata ushindi ndani ya dakika 90 kwenye mechi sita.
Stars juzi Jumatatu iliendelea kushindwa kutamba baada ya kuambulia suluhu mbele ya Rwanda pale Kigali, Rwanda ukiwa mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Fifa.
Mrundi huyo ameisimamia Stars kwenye michuano tofauti kwa dakika 540, ambazo sawa na mechi sita baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mnigeria Emmanuel Amunike.
Katika mechi hizo ambazo amesimamia kocha huyo kwenye mashindano tofauti ndani ya dakika 90, hakuna mchezo hata mmoja ambao aliondoka na ushindi.
Mrundi huyo ameisimamia Stars katika mechi sita ndani ya dakika 90 licha ya kushindwa kuibuka na ushindi lakini ndani ya dakika hizo yamefungwa mabao mawili pekee na wakiruhusu mabao matatu.
Kocha Ndayiragije tangu apewa timu hiyo amesimamia mechi zifuatazo; Stars 0-0 Kenya, Kenya 0-0 Stars. Burundi 1-1 Stars, Stars 1-1 Burundi, Stars 0-1 Sudan na Rwanda 0-0 Stars.
Mechi 6
Mabao ya kufunga 2
Mabao ya kufungwa 3
Ushindi dk 90 hakuna
Kupoteza mechi 1
0 comments:
Post a Comment