Yanga inatua Mwanza leo Ijumaa na uongozi wa matawi yao jijini hapa umewaandalia mapokezi ya maana.
Katibu mkuu wa matawi hayo, Mhando Madega amesema; “Tulikuwa na kikao na viongozi wa matawi ya Yanga jijini Mwanza kwa pamoja tumeazimia kuipokea timu yetu kwa mapokezi makubwa ikiwa ni ishara ya kufanya vyema katika michezo yetu miwili dhidi ya Mbao na Pyramids.”
“Licha ya kuandaa mapokezi makubwa lakini sisi hatulali tunapambana ili Yanga yetu iweze kupata matokeo ya hii michezo miwili.
"Endapo tutafanya vizuri katika michezo yetu yote tutajenga imani kubwa kwa viongozi wetu wa juu waendelee kutuamini ili hata michezo mingine waweze kuileta katika jiji la Mwanza ambako tunapata matokeo,”alisema.
0 comments:
Post a Comment