Kwa sasa Arsenal ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15, wakati vinara wa ligi Liverpool wakiwa na alama 24, Man City ikishika nafasi ya pili kwa pointi 16.
Nyota wa zamani wa Manchester United na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham anammendea mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kuwa mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya uwakala wa wachezaji. (Mail)
Miamba
ya soka nchini Hispania, Real Madrid imehusishwa kutaka kumsaini kiungo
wa kati wa Denmark, Christian Eriksen dirisha lijalo la usjili la mwezi
Januari.(Marca)
Klabu hiyo pia wanaisaka saini ya mshambuliaji
kinda wa Red Bull Salzburg mwenye umri wa miaka 19, raia wa Norway,
Erling Haaland ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester
United. (AS)Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast, Serge Aurier 26, amesema kwamba alitaka kuondoka mjini London mwishoni mwa msimu uliopita na kukiri kuwa mpaka sasa hajui hatma yake iko vipi katika klabu hiyo. (Football.London)
Aston Villa imehusishwa na kutaka kusaini ya kiungo wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)
0 comments:
Post a Comment