Thursday, October 10, 2019



Ni kama hofu imetanda kwa mashabiki wengi wa Yanga kutokana na droo iliyofanyika usiku wa jana katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Jana Yanga ilipangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC ya Misri katika hatua ya Play-Off ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Baada ya droo hiyo, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameonekana kuwa na uoga kutokana na takwimu za Pyramids ambayo imeshika nafasi ya pili kunako ligi hiyo.

Mbali na kuwa nafasi ya pili, timu hiyo pia imesajili wachezaji ghali zaidi ambapo baadhi yao wamegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni moja.

Yanga itaanza safari yake hapa nyumbani kucheza na Pyramids Oktoba 27 kabla ya kwenda ugenini kurejeana nao Novemba 03 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment