Saturday, October 5, 2019



Winga wa miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus, Douglas Costa amempongeza mchezaji wa Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC, Fraga Vieira kwa kuongeza mwaka mwingine katika siku yake ya kuzaliwa.

Loading...
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Douglas Costa amemtumia ujumbe mfupi beki huyo Simba baada ya kuweka picha yake ambayo akionekana akimwagiwa maji na wachezaji wenzake wa Msimbazi.

Douglas Costa de Souza akiwa na Ronaldo

Douglas Costa de Souza amempongeza nyota huyo kwa kuandika kuwa ”Caraleo, umekuwa 👴 !  nakumbuka ukiwa chini ya miaka -15 Gerson 😂😂😂 hongera shujaa,”  amesema mchezaji huyo wa Juventus.


Fraga Vieira raia wa Brazil amesajiliwa Simba SC akitokea katika klabu ya ATK FC ya India kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo mwenye ambaye sasa anatimiza miaka 27 ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Brazil ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 iliyokuwa na wachezaji maarufu kama vile Neymar, Philippe Coutinho na Casemiro.

0 comments:

Post a Comment