Tuesday, December 24, 2019



Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anaamini VAR inaua ligi bora duniani baada ya kile kilichotokea katika mechi yao dhidi ya Chelsea juzi Jumapili.

Nyota wa Spurs Son Heung-Min alipigwa kadi nyekundu dakika ya 62 kwa kuonekana kumchezea rafu beki wa Chelsea Antonio Rudiger katika mchezo huo ulioisha kwa Spurs kupoteza kwa goli 2-0 wakiwa uwanja wa nyumbani.

Awali mwamuzi wa mchezo Anthony Taylor hakuona kosa lolote mpaka pale ilipoingiliwa na mwamuzi msaidizi wa video (VAR) Paul Tierney ndipo kadi nyekundu ikatolewa.

“Kwa tukio la Son, ninafikiri Bw.Tierney alikosea. Ni kosa," Mourinho aliwaambia waandishi wa habari

“Hii ni England,ni Premier League, mashindano bora zaidi duniani, yenye sifa ambazo kama tutazibadili, tunaiua ligi bora zaidi duniani”

“Paul Tierney anaamua ndio na Anthony Taylor, katika muda sahihi, mita tano kutoka kwenye tukio, aliamua si (kadi nyekundu) . Kwa hiyo ni nani alikuwa anachezesha mechi? Si Bw.Taylor. Ilikuwa ni Bw.Tierney”

“VAR inatakiwa kuunga mkono mpira wa miguu, kuleta ukweli kwa (mchezo). Walifanya hivyo kwa maamuzi ya penati na wakaua mchezo na maamuzi ya Son”

 Hata hivyo klabu ya Tottenham tayari wamekata rufaa kupinga kadi hiyo nyekundu aliyopata Son.

0 comments:

Post a Comment