Tuesday, December 24, 2019



Kocha wa Tottenham, Jose Mourinho, amesema sasa anataka mastaa wake, beki Jan Vertonghen na kiungo Christian Eriksen wasaini mkataba, hii ni siku chache baada ya kumsainisha mkataba mpya beki aliyekuwa akitaka kuondoka, Toby Alderweireld.

Vertonghen na Eriksen wote mikataba yao inafikia tamati mwishoni mwa msimu huu huku Eriksen, akiwa na shauku kubwa ya kuondoka klabuni hapo baada ya msimu. Alderweireld yeye aliamua kusaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kushawishiwa na Mourinho.

0 comments:

Post a Comment