Tuesday, December 24, 2019



Uwepo wa Ghalib Mohammed katika kampuni ya GSM ndani ya Yanga unaonekana kudhamiria kuiboresha timu hiyo kwa kasi ambapo inaelezwa hivi sasa wanapambana kuwania saini ya winga wa TP Mazembe.

Tetesi zinasema kuwa mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara zinasema kuwa Yanga wameanza kuwania saini ya winga Gnanzou Djeni.

Winga huyo kutoka taifa la Ivory Coast ameanza kuvutiwa waya na Yanga ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwa muda mrefu ndani ya kikosi hicho.

Kukosa namba kwa mchezaji huyo kumemfanya awe katika mikakati ya kutaka kuhama ili aelekee mahala pengine kwa ajili ya kulinda kipaji chake.

Sababu hizo zinawafanya Yanga wazidi kutia nguvu ili kupata saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kuja kuboresha kikosi cha Yanga ambacho kimekuwa kikifanya usajili wa wachezaji wapya.
24Dec2019

0 comments:

Post a Comment