Tuesday, December 24, 2019



Licha ya awali kuelezwa kuwa mabosi wa Yanga wanapamba kunasa saini ya mchezaji, mshambuliaji kutoka UD do Songo, Luis Muquissone, inaelezwa Simba wako katika hatua za mwisho kumalizana naye.

Mchezaji huyo ambaye aliwafunga Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika raundi ya mchezo wa pili, amekuwa katika vichwa vya habari vingi nchini juu ya timu za Simba na Yanga.

Taarifa zinasema kuwa vigogo kadhaa wa Simba walishasafiri kuelekea Msumbiji kuweka mikakati kadhaa kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Licha ya wanayanga wengi kuamini kuwa mchezaji huyo anaweza kutua kwao, hali inazidi kuwa tofauti kutokana na kuendelea kubadilisha upepo na inaonesha zaidi ya asilimia 95 anaweza kutua Simba.

0 comments:

Post a Comment