ROMELU Lukaku, nyota wa Inter Milan amesema kuwa Paul Pogba alikuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Manchester United kumwambia kwamba ameamua kuondoka ndani ya kikosi hicho.
Lukaku mwenye miaka 26 alisepa ndani ya United baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili kwa kile alichoeleza kuwa kilitokana na kubadilishiwa majukumu ndani ya uwanja.
Raia huyo anayekipiga timu ya taifa ya Ubelgiji pia aliondoka kwa dau la thamani ya pauni milioni 73 na alikuwa na urafiki wa karibu na Pogba alipokuwa ndani ya United.
"Nilimwambia Pogba kwamba tayari nimeshakamilisha dili mapema kabla ya kuwaambia watu wengine ndani ya United, ndio yeye alikuwa mtu wangu wa karibu muda wote na siku zote," amesema Lukaku.
0 comments:
Post a Comment