Mrembo
wa Kirusi mwenye mvuto wa aina yake, Viktoria Odintcova, amedai kuwa
aliikaushia na kuifutilia mbali meseji aliyotumiwa na supastaa Cristiano
Ronaldo baada ya fowadi huyo wa Juventus, kumtumia ujumbe Instagram.
Mrembo
huyo, 34, mwenye wafuasi milioni tano kwenye Instagram, amefunguka kuwa
aliitosa meseji ya staa huyo miezi kadhaa iliyopita.
“Aliniandikia ujumbe mfupi. Ilikuwa ni zamani kidogo. Aliandika hivi, “Mambo, mzima wewe?”
“Nilifuta meseji hiyo na sikujibu,” alisema mrembo huyo.
Aliongeza: “Sikutaka kumpa nafasi, kwa sababu nawajua wanawake wengine aliowaandikia, kwa hiyo nilielewa lengo lake mapema.”
Ronaldo kwa sasa yupo penzini na mrembo Georgina Rodriguez tangu 2016 na wana mtoto mmoja wa kike pamoja aitwaye Alana.
0 comments:
Post a Comment