Kuna
uwezekano mkubwa mshambuliaji mpya wa Yanga, Ditram Nchimbi, anaweza
asiwe sehemu ya mchezo dhidi ya watani wa jadi Simba, Januari 4 2020.
Yanga
ilimtambulisha mchezaji huyo ambaye alikuwa kwa mkopo Polisi Tanzania
wakati akiwa ana mkopo na Azam kwa kuingia naye mkataba.
Taarifa
zinasema kuwa mabosi wa Polisi Tanzania wametuma barua kwenda TFF
wakieleza kuwa kuna makubalinao maalum waliingia na Azam baada ya
kumchukua kwa mkopo.
Polisi
wanadai kuwa makubaliano hayo ni kama yamekiukwa mpaka imepelekea
Nchimbi akaelekea Yanga kitu ambacho wao wanadai kuna baadhi yamekiukwa.
Kinachosubiriwa
hivi sasa kwa TFF ni kutoa tamko juu ya Nchimbi ambaye kama mambo
hayatakuwa sawa anaweza kuikosa mechi dhidi ya Simba.
0 comments:
Post a Comment