MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa amefurahishwa na uwezo wa vijana wake ndani ya Uwanja ana imani watafanya makubwa ndani ya mwaka mpya wa 2020 kwenye mechi zao zote.
Arteta amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kuimarika na kushinda mbele ya Manchester United bali jitihada za wachezaji kwa kujituma ndani ya uwanja zimeleta matokeo.
"Sio kazi nyepesi kupata ushindi kwenye mechi zetu za ligi kwani timu zote ni bora na kila mmoja amejipanga kufanya vizuri, tunapambana na tunajua kwamba tuna kazi kubwa ya kufanya," amesema.
Arsenal imepata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Manchester United mbapo ni ushindi wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Arteta akiwa na Arsenal baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi akipokea mikoba ya Unai Emery ambaye alitimuliwa.
0 comments:
Post a Comment