Tuesday, December 31, 2019


Desemba 10, 1987 alizaliwa mchezaji soka wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Juventus ya Italia Gonzalo Higuain ‘El Pipita’ ambaye hucheza katika nafasi ya ushambuliaji.

Alizaliwa katika mji wa Brest nchini Ufaransa kwa baba ambaye alikuwa mchezaji wa soka Jorge Higuain ambaye wakati huo alikuwa akiitumikia klabu ya Stade Brestois 29. Ni miongoni mwa vizazi vya Basque kwa upande wa baba yake. Aliondoka nchini Ufaransa baada ya miezi 10 hivyo hawezi kuongeza kifaransa licha ya kuwa kuwa na uraia wa Ufaransa na Argentina ambao aliupata mwaka 2007.

 Higuain ana kaka zake wawili Nicolas na Federico ambaye anahudumu katika Ligi Kuu nchini Marekani katika klabu ya Columbus Crew pia ana mdogo wake anayefahamika kwa jina la Lautaro. Alipewa jina la El Pipita au Pipa na baba yake Mzee Jorge. Alianza kucheza soka katika klabu ya River Plate klabu ya kutua Real Madrid Januari 2007 kwa ada ya euro milioni 12.

Akiwa nchini Hispania alitwaa vikombe vya ndani ikiwamo mataji matatu ya La liga na kufunga mabao 107 katika mechi 190 alizocheza.


Baada ya hapo alijiunga na Napoli kwa ada ya euro milioni 40 Julai mwaka 2013  ambako alishinda Coppa Italia katika msimu wake wa kwanza.

Msimu wa 2015-16 alifunga mabao 36 katika serie A na kutwaa tuzo ya Capocannoniere hivyo akaweka rekodi ya kuwa sawa na nyota mwingine aliyewahi kufanya hivyo Gino Rossetti.

Kutoka na rekodi hiyo mabingwa wa Serie A Juventus walimsaini nyota huyo mnamo mwaka 2016 kwa ada ya euro milioni 90 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Amerika Kusini kusajiliwa kwa ada kubwa hadi ilipokuja kuvunjwa mwaka 2017 wakati wa Neymar akitua PSG.

0 comments:

Post a Comment