MERIH Demirah, beki wa Juventus ameingia kwenye rada za kuwindwa na Arsenal iliyo chini ya Mikel Arteta.
Bosi huyo mpya ndani ya Arsenal amesema kuwa anahitaji kuongeza nguvu kubwa kwenye safu ya ulinzi ili kuimarisha kikosi chake.
Mpaka
sasa Arsenal imefungwa jumla ya mabao 30 ndani ya Ligi Kuu England
jambo linalomtisha kocha huyo aliyewatungua Manchester United mabao 2-0
na ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo.
Licha
ya David Luiz na Kieran Tierney kusaini ndani ya Arsenal msimu uliopita
bado hawajawa na safu imara ya ulinzi jambo linalomfanya Arteta
kumfikiria Demiral mwenye miaka 21 kujibu tatizo la safu yake ya ulinzi.
Akiwa Juventus iliyo chini ya Maurizio Sarri alianza kwenye mechi nne za mwisho za kikosi hicho hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment