Friday, January 3, 2020



MIRAJ Athuman, 'Sheva' nyota wa Simba ambaye ni super sub ndani ya kikosi hicho kesho hatakuwa sehemu ya timu itakayomenyana mbele ya Yanga.

Yanga itakaribishwa kesho, Januari, 4 kwenye Uwanja wa Taifa kumenyana na Simba mechi itakayokuwa na mvuto kutokana na ushindani uliopo.

Sven Vanderbroek, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa Miraj ataukosa mchezo huo kutokana na majeruhi.

"Kikosi kipo tayari isipokuwa kwa Miraji na Rashid (Juma) ambao wana majeruhi lakini waliobaki wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Yanga," amesema.

Sheva ana mabao sita ndani ya Simba na asiti moja alisababisha jumla ya penalti mbili ndani ya Simba zote zilifungwa na Meddie Kagere.

0 comments:

Post a Comment