UONGOZI
wa Klabu ya Singida United umetangaza kuingia mkataba wa miezi sita na
wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’, Haji mwinyi aliyekuwa KMKM ya Zanzibar
na Tumba Lui ili kukiongezea nguvu kikosi hicho kilicho mkiani mwa
msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Singida
mpaka sasa imeshakamilisha usajili wa wachezaji sita ikiwa ni katika
harakati ya kukinusuru kikosi hicho kinachoonekana kuwa dhoofu msimu
huu.
Ofisa
Habari wa Singida United, Cales Katemana, amesema kuwa bado wanaendelea
kukiimarisha kikosi chao kuendana na mapendekezo ya kocha, Ramadhan
Nswanzurimo.
“Tunaendelea
kufanya usajili kuendana na mapendekezo ya mwalimu na hivi
tumekamilisha usajili wa Boban na wenzake ambao wamejiunga nasi kwa
mkataba wa miezi sita.
“Kwa
sasa tumeweka nguvu katika kusajili wachezaji wenye uzoefu kwa kuwa
tunaamini kwa uzoefu walionao wataisaidia timu kufanya vizuri kwenye
michezo yetu ijayo,” amesema Katemana.
0 comments:
Post a Comment