Manchester United
inajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kwa Real
Madrid au Juventus mwezi huu, lakini wanataka £150m. (Express)
Manchester
United inapania kuwanunua viungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish,
24, na James Maddison, 23, kutoka Leicester. (Independent)Wachezaji wengine wanolengwa na United ni kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can, 25, na Sean Longstaff, 22, wa Newcastle. (ESPN)
Aston Villa ina mpango wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudmu. (Footmercato - in French)
Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Sun)
Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ameelezea kujitolea kwake kwa Arsenal na kutuliza tetesi za kuondoka kwake mwezi Januari. (Evening Standard)
Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Telegraph)
Inter Milan ni moja ya klabu zilizowasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen. Kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 27 inakamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Manchester City inatarajiwa kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34. (Sun)
Dau la Chelsea la yuro milioni 40 la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele ,23, limekataliwa na Lyon. (Footmercato - Kwa Kifaransa)
Aston Villa inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua kipa wa Stoke City Muingereza, Jack Butland, 26. (Mail)
Ajax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen kwa sababu bei ya mchezaji huyo wa miaka 32 ni ghali sana . (De Telegraaf - Ujerumani)
Southampton wanataka kumsaini beki wa Valladolid raia wa Ghana Mohammed Salisu, 20. (Sky Sports)
Leicester imeipiku Arsenal katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Juventus na Italia, Daniele Rugani, 25. (Express)
Arsenal imemuulizia winga wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Marca - ya Uhispania)
Tetesi Bora Alhamisi
Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)
0 comments:
Post a Comment