Friday, January 3, 2020



Klabu ya Simba imemalizana na kiungo wa kimataifa wa msumbiji Luis Jose Miquissone ambaye alikuwa akichezea klabu ya UD Songo kwa mkopo.
Luis ndiye aliyeifungia UD Songo bao dhidi ya simba kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika uliopigwa Jijini Dar es Salaam mwezi septemba mwaka jana  na kulazimika kwa sare ya 1-1  matokeo ambayo yaliwatupa simba kwenye michuano.
 Kiungo huyo amekabidhiwa jezi  ya timu hiyo na kocha wa timu hiyo Sven Vandenbroeck

Kocha Mbelgiji wa Simba SC, Sven Vandenbroeck akimkabidhi jezi kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone baada ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na klabu hiyo akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo msimu huu ilimpeleka kwa mkopo UD Songo ya kwao

0 comments:

Post a Comment