Friday, January 3, 2020


OBREY Chirwa, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa ushindani kwenye ligi unaifanya timu yake kupambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zote.

Chirwa amefunga jumla ya mabao manne ndani ya Azam FC msimu huu akiwa ametoa asisti moja ya bao ni miongoni mwa wachezaji waliofunga 'hat trick' msimu huu kwenye ligi.

Chrwa amesema :" Kila timu inapambana kupata matokeo na kwa sasa kilichobaki ni kuona namna gani timu itafikia malengo iliyojiwekea.

"Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi kubwa inakuja mbele kutokana na kila timu kujipanga," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 13 ina jumla ya pointi 26 kibindoni.

0 comments:

Post a Comment