Friday, January 3, 2020



CHARLSE Mkwasa,Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ushindi wao mbele ya Tanzania Prisons unawapa matumaini ya kufanya makubwa kwenye mechi ya kesho dhidi ya Simba.

Mkwasa amesema kuwa kwenye mechi zao tano za hivi karibuni walizocheza waliweza kuifunga kwa mara ya kwanza Tanzania Prisons jambo hivyo hawana hofu na Simba zaidi ya kuwaheshimu.

"Tumecheza mechi nyingi ngumu na tumeweza kupata matokeo, mbele ya Tanzania Prisons ambayo ilikuwa haijafungwa tuliifunga hivyo tunaweza kupata matokeo chanya mbele ya Simba.

 "Timu ya Simba ni nzuri na ninaiheshimu tutapambana kupata matokeo mashabiki, wajitokeze kutupa sapoti kwenye mechi yetu hiyo," amesema.

Tanzania Prisons ilicheza jumla ya mechi 12 bila kufungwa mechi ya kwanza ilipoteza mbele ya Yanga mechi yake ya 13 kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Samora bao pekee la Patrick Sibomana. 

0 comments:

Post a Comment