BEKI wa Manchester United, Ashley Young imeripotiwa kuwa amegomea mazoezi ya timu yake akishinikiza kutimkia ndani ya kikosi cha Inter Milan.
Young
amekubali kujiunga na Inter Milan inayoshiriki Serie A akitokea kwenye
timu inayoshiriki Ligi Kuu England na anatarajia kufanyiwa vipimo hivi
karibuni kukamilisha dili hilo.
Imeripotiwa
kwamba nyota huyo hafurahishwi na maisha yake ndani ya Manchester
United na mabosi wa Inter Milan wameweka mezani pauni milioni 15 kuipata
saini yake.
Nyota
huyo amegomea dili la kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya United
na anahitaji kuondoka kwenye usajili wa mwezi Januari licha ya mkataba
wake kumeguka mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment