JURGEN
Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa alimaliza mapema mgogoro wa
nafsi kati ya Mohamed Salah na Sadio Mane uliotokea ndani ya timu yake
mwezi Agosti,2019.
Mshambuliaji Sadio Mane alionekana kumlalamikia Salah kwa kushindwa kumpa pasi ya wazi wakati akitoka alipofanyiwa mabadiliko.
Kwenye
mchezo huo dhidi ya Burney uliochezwa Uwanja wa Turf Moor, Salah
aliamaua kupiga shuti badala ya kutoa pasi na timu yake ilishinda mabao
3-0.
Klopp
amesema kuwa:" Kwenye mpira kuna maajabu sana unaweza kumtazama
mchezaji namna anavyofanya na ukapata maneno rasmi anayoongea, niliona
kama Mane amesema 'Ohh kwa nini umeamua kufanya hicho ulichofanya,? ila
ni maisha ya mpira na yote lazima yatokee.
"Haikunichukua
muda mrefu baada ya mechi nilikaa nao wote na nikazungumza nao kwa
muda usiopungua dakika 15, na sasa unaona wana furaha na masiha
yanaendelea," amesema.
0 comments:
Post a Comment