Friday, January 17, 2020


MTIBWA SUGAR: HAIKUWA BAHATI YETU LEO, YAFUNGWA MABAO 2-0 NA KMC
SADALA Kipangwile, leo amekuwa nyota wa mchezo kwa KMC kwa kupeleka kilio mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru, leo Januari,17,2020.

Kipwagile alipachika baao la kwanza dakika ya 18 na lile la pili alipachika dakika ya 43 na kuifanya timu yake ishinde kwa jumla ya mabao 2-0.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kila timu ilipambana kutafuta matokeo mwisho wa siku ushindi ukawa kwa KMC.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa haikuwa bahati yao kupata ushindi mbele ya KMC.

0 comments:

Post a Comment