Uongozi wa klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) umeingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu (miezi 18) na kocha Haruna Harerimana raia wa Burundi baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kuinoa timu hiyo.
Harerimana anachukua nafasi ya kocha Jackson Mayanja kutoka Uganda ambaye mkataba wake ulisitishwa kutokana na timu hiyo kutokuwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya Kimataifa.
Harerimana ambaye alikuwa akiinoa Lipuli FC tangu kuanza kwa msimu huu, amepitishwa na bodi ya KMC baada ya kupitia maombi mengi ya makocha wa ndani na nje ya nchi.
Kocha Harerimana ametambulishwa kwa wachezaji na tayari ameanza kazi ya kuinoa timu ya KMC kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
“Ni kocha ambaye amekidhi vigezo vyote ambavyo tumeweka na uongozi kuamua kuingia naye mkataba. Kupitia yeye, tunaamini timu itafanya vyema na kurejesha ubora wake wa msimu uliopita,” amesema Mwenyekiti wa Bodi ya timu ya KMC, Meya Benjamin Sitta.

0 comments:
Post a Comment