Friday, January 3, 2020


Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kuwa yeye huwa aropoki bali anaongea ukweli ila mashabiki wa Yanga wanamugopa sana, wanatetemeka na wengine wanatamani hadi afe pale wamuonapo ila ndiyo hivyo hawana cha kumfanya.

Akipiga stori leo kwenye vituo mbali mbali vya habari haji manara ameonekana mwenye kujiamini sana katika mchezo dhidi ya yanga utakaopigwa kesho na kudai kubwa simba ni baba lao.

"Nitajie neno moja ambalo unaona nimeropoka, baadhi ya mashabiki wa Yanga ndiyo wanasema naropoka sio watu, tena wanaotoka mitandaoni wapuuzi wanasema mimi naropoka sasa si ningekamatwa na polisi yaani niropoke halafu Serikali iniache, Yanga huwa wanajiona  wakubwa na hawaguswi wanataka wawatanie Simba halafu wao wasitaniwe" amesema HajiManara.

Haji Manara ameongeza kuwa "Vyote ninavyoongea nina uhakika navyo hakuna hata kimoja nisichokuwa na uhakika, tangu nimeanza kuwa boksi Yanga wananiogopa halafu hawana cha kunifanya hata nikitokea wanatetemeka na wengine wanatamani nife".

Siku ya Januari 4, 2020, kutakuwa na mchezo wa ligi kuu kati ya timu yake ya Simba dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, utakaochezwa majira ya saa11:00 jioni, katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment