Sander Berge amfuata Samatta kwenye ligi kuu ya Uingereza Klabu ya Sheffield United imevunja rekodi yao ya usajili kwa kumsajili kiungo rai wa Norway Sander Berge kwa £22m kutoka klabu ya Genk ya Ubelgiji. Berge mwenye miaka 21 ambaye amecheza tayari michezo 20 kwa nchi yake amesaini mkataba hadi 2024 kuitumikia Sheffield United.
0 comments:
Post a Comment