Kocha
wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema mabadiliko aliyokuwa anafanya
kupanga kikosi kipya kila mchezo, alikuwa anatunza nguvu kwa wachezaji
wake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga,
unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi ya time yake na Ndanda FC,
kocha huyo alisema kumpumzisha Meddie Kagere, Pascal Wawa na Clatous
Chama ni kuwapa muda kwa ajili ya kujipanga na mchezo ujao.
“Tuna
mchezo mgumu dhidi ya Yanga na tunahitaji ushindi, hivyo niliwapumzisha
Meddie Kagere, Pascal Wawa na Clatous Chama ili wajipange kwa mchezo
ujao,” alisema Sven.
Kocha
huyo amefurahishwa na ujio wa beki kiraka Erasto Nyoni na nahodha John
Bocco na kuonesha kiwango bora kwenye mchezo huo, akiamini siku zijazo
atakuwa na kikosi bora zaidi cha ushindani.
Aidha,
aliwapongeza wachezaji, Deo Kanda na Francis Kahata, kwa kufunga mabao
yaliyoifanya timu hiyo kuibuka na ushindi na kuzidi kuwaweka kileleni
mwa msimamo wa ligi na katika mbio za kutetea ubingwa.
Alisema
kwenye mchezo dhidi ya Ndanda FC walicheza mpira wa kufunguka zaidi,
lakini wapinzani wao waligundua mbinu hiyo na kushindwa kufuata mfumo
wao hivyo kucheza taratibu kupoozesha kasi yao.
“Baada
ya kutokea hali hiyo, nilifanya mabadiliko kwa kumwingiza Deo Kanda na
Chama walioongeza nguvu na kupata bao la pili,” alisema Sven.
Naye
kocha wa Ndanda FC, Abdul Mingange, alikubali matokeo na kusema muda
mwingi walikuwa wanapoozesha mchezo na kucheza kwa kujilinda ili
kupunguza idadi ya mabao.
“Tuliingia
na mbinu ya kujilinda kupunguza idadi ya mabao na kweli tulifanikiwa
lakini tungesema tufunguke wangetufunga mabao mengi kwa kuwa wapinzani
wetu wana kikosi bora, “ alisema Mingange.
Simba
inaongoza ligi ikiwa na pointi 34 na Ndanda ina pointi nane ikiwa
katika nafasi ya 18 ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment