Friday, January 3, 2020



Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake Haji Manara, umesema utaingia na mabakuli zaidi ya 30 katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam ili kuwachangia Yanga.

Manara ameeleza mabakuli hayo yatatumiwa na mashabiki wa Simba kuchangia fedha hizo ili waweze kuwapatia Yanga baada ya mechi.

Ameeleza kuwa wao na Yanga ni watani wa jadi pia ni ndugu na huwa wanazikana hivyo hakuna haja ya kushindwa kusaidiana.

Manara amefunguka akieleza wamedhamiria kufanya hivyo ili kuwasaidia fedha kadhaa ambazo zitasaidia kulipa mishahara ya wachezaji wa Yanga sambamba na kutimizia majukumu mengine.

0 comments:

Post a Comment