TIMO Werner, mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig na timu ya Taifa ya Ujerumani ameziingiza vitani Manchester United, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich ambazo zinasaka saini yake.
Nyota
huyo amekuwa na uwezo mkubwa ndani ya Uwanja jambo ambalo linawavutia
mabosi wa timu nyingi na huenda kwenye dirisha hili lililofunguliwa
mwezi Januari akasepa jumla na kwenda kati ya timu hizo.
Habari
zinaeleza kuwa timu nyingi mbali na Chelsea ambazo zinashiriki Ligi Kuu
England zinamuelewa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23.
Anasifika
kwa kucheza namba 10 ndani ya uwanja na amefunga jumla ya mabao 24 kwa
ujumla ndani ya timu yake ya Taifa pamoja na klabu yake inayoongoza
Bundesliga ikiwa na pointi 37.
0 comments:
Post a Comment