Thursday, January 2, 2020


NIKIWA safarini kwenda nje kabisa mwa jiji mashuhuri hapa nchini kwetu.jiji la Dar es salaam jiji ambalo nimezaliwa na kukulia hapa hadi kufikia umri huu niliokuwa nao.
Safari hii ilikuwa ni ya kuelekea moja ya kijiji katika mkoa wa pwani kijiji  Kinachoitwa 'Kingono Ngono' kwenda kumsalimia Ndugu yangu niliye potezana naye kwa mda mrefu saana kutokana na shughuli za kila siku za kulimbiza tonge la ugali.๐Ÿ˜Œ
Nikiwa safarini nilipokea kwa moja ya marafiki zangu ambaye anafanya kazi ya uchambuzi katika moja ya kituo cha redio hapa nchini ambaye alikuwa ananijulisha kuwa  Mpaka mda huo yanga tayari ilisha sajili wachezaji takribani watatu ambao woote wana mlengo wa kuwaona wakionesha kitu kwenye mechi ya tarehe Nne.

Moyoni mwangu niakaona kuna kaa la moto lililonichoma vilivyo na kunambia kuwa hapa kuna kitu cha kuandika kupitia usajili huu.
Sikuwa nimetulia kwenye kiti nilichokuwa nimekaa hata ikamfanya abiria mwenzangu niliyekaa naye kuniuliza mbona nahangaika saana.nikamwambia nina kaa la moto lina nichoma moyoni na dawa yake mpaka nilitoe na kulitoa kwake lazima niandike yaliyo moyoni kuhusiana na usajili huu unaofanywa na hawa tunao waita wakubwa wa mpira.
Ili kunisaidia abiria yule alinipa peni na karatasi ili kutoa kile ninachotaka kukiandika kuhusiana na usajili huo.
"Kwako  Master Mkwasa pole sana kwani najua kwa sasa kichwa chako hakina hata vugu vugu la ubaridi kwani joto litokalo tumboni mwako kuelekea tarehe nne linaweza hata kulainisha chuma.
Najua joto linakuzidi zaidi baada ya kukumbuka Taswira ya goli la Tariq seif huku Mzimu wa Ditram Nchimbi ulio ipeleka Tanzania kwenye michuano ya CHAN bado nao unaendelea kukuandama.
Najua hesabu za kukipanga kikosi cha kwanza ndizo zinazofanya ung'ate peni yako kwa kufikiria tu.
Unafikiria una Tariq,Yikpe,Ditram na Molinga ambao wote wanaweza kucheza namba tisa wakati huo namba kumi tayari imeshapata mtu ambae ni  Tshishimbi je nani kati ya hawa atacheza na Tshishimbi iyo tarehe nne? Najua hili ni swali ambalo bado linakundam kichwani mwako.
Ikiwa Haruna naye anacheza namba 11 huku nane na Sita zikiwa ni mali ya watoto wa Kibrazili kutoka Visiwani Nzanzibar ambao ni Makame,Feisal na Mo banka.huku namba saba ukimuangalia Kaseke ama Ngassa.
Najua unajiuliza je kati ya hawa washambuliji woote wanne nani atakuwa sahihi kuanza katika mecho hiyo.huku akilini mwako ukiwa unajiuliza ikiwa ataanza Tariq seif na asipopata goli kipindi cha kwanza je? Ukimtoa hatokuwa amepoteza confidence? Au akianza Yikpe naye alafu akatoka kipindi cha pili haitokuwa imemshushia hali ya kujiamini?
Najua mtihani mkubwa unao kujia kichwani ni hasa unapo angalia hawa washambuliaji wako wanne na kuwaza nani aanze na nani aanzie benchi je akianzia benchi haito muathiri?
Hakika nikupe pole kwakuwa moyo wako unalia kwakuhisi kuna msiba lakini cha  marehemu ndiyo msababishaji.
Ntakuja kuongelea tena mecho hii kwa ujumla kabla ya mecho yenyewe lakini hapa nimejaribu kuielezea  hali hii anayopitia Mkwasa.
Nimeanza kwa mda mchache saana kuandiika kwenye tovuti hii lakini mapenzi yenu yalinishangaza tokea siku ya kwanza naanza kuandika hakika mumenifanya nizidi kupata matumaini mapya pale tu nionapo jumbe zenu za kunisifia ziwe na ela ya soda basi๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ, na kunipongeza japo  mialiko sikupata christmass๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚  bado nawashukuru sana.

0 comments:

Post a Comment