Monday, February 3, 2020

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amedai kuwa klabu hiyo “isingekubali kutapeliwa” baada ya kushindikana usajili wa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani. (ESPN)

Image result for Edinson Cavani to united"
Kocha wa Lazio alia na Giroud adai angempata ndoto zake za Ubingwa zingetimia, Cavani aisumbua Atletico Madrid ayakataa mamilioni ya United
Cavani
Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham amesikitishwa na klabu yake kushindwa kumsajili Cavani. (Mirror)
Timu inayomilikiwa na mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham Inter Miami iliyopo Marekani inataka kuongeza nguvu ya kumsajili Cavani pale mkataba wake na PSG utakapofika tamati mwishoni mwa msimu. (L’Equipe)
Cavan mwenye umri wa miaka 32, huingiza paundi 360,000 kwa wiki kutoka kwa matajiri hao wa Ufaransa lakini mwenyewe ameamua kukatwa kiasi hiko cha pesa ili kuwezesha yeye kuondoka PSG.
Ndugu wa mchezaji huyo amesema yupo yari kuona anapunguziwa pato lake ili tu kutimka “Cavani yupo tayari kupata kiasi kidogo kutoka kwa PSG,” amesema Walter Guglielmone kaka wa Mshambuliaji huyo.
Walter Guglielmone ameongeza kuwa Edi haja ingia uwanjani kucheza kwa mwezi mmoja ”Kama angekuwa yupo kwaajili ya pesa basi angeenda England, ndani ya Manchester au Chelsea.”
Willian
Willian amekuwa akihusishwa na Barcelona kwa muda mrefu sasa
Winga raia wa Brazil Willian, 31, angependelea kusaini mkataba mpya utakaombakiza Chelsea kuliko kujiunga na mabingwa wa Uhispania Barcelona. (ESPN)
Barcelona wametupilia mbali ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli Fernando Llorente, 34. (AS)
Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka kusajili kipa mpya baada ya kuporomoka kiwango cha kipa Kepa Arrizabalaga, 25. (Express)
Kiungo Mesut Ozil, 31, alipewa nafasi ya kuihama Arsenal mwezi uliopita na kocha wake Mikel Arteta alikuwa tayari kumruhusu. (Mirror)Ozil
Ozil amekuwa na wakati mgumu Arsenal kwa kipindi kirefu sasa.
Kiungo wa Lille Boubakary Soumare, 20, almekataa ofa nono ya kujiunga na klabu ya Newcastle mwezi Januari akiamini kuwa anaweza kujiunga na Liverpool ama Manchester United mwishoni mwa msimu. (Le10sport – in French)
Liverpool wanajipanga kumsajili mshambuliaji kinda na machachari wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 19, mwishoni mwamsimu. (Express)Giroud
Giroud amesalia Chelsea licha ya kufuatiliwa na vilabu kadhaa.
Kocha wa Lazio Simone Inzaghi amesema laiti angelimpata mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, kungewezesha ndoto zake za kufukuzia ubingwa kuwa na “machaguo zaidi.” (Gazzetta)
Kocha Roy Hodgson ameionya bodi ya Crystal Palace kuwa watakuwa na kazi ngumu ya kuboresha kikosi chao mwishoni mwa msimu. (Standard)
Hodgson, ambaye anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu anaitaka klabu hiyo kufikiria namna bora ya kuendelea nayo baada ya kushindwa kufurukuta kwenye dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Telegraph)

0 comments:

Post a Comment