KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila
amesema kuwa timu ya Sahare Stars ipo vizuri na ikipambana itafikia
malengo iliyojiwekea.
Sahare iliwanyoosha Mtibwa Sugar kwenye
mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora kwa kuwaondoa kwenye reli
vigogo hao wanaoshiriki Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa penalti 3-2 baada
ya kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.
Katwila amesema kuwa walicheza vizuri na walionyesha ushindani jambo lililowapa nafasi ya kusonga mbele.
"Tulikuwa na changamoto kutoka kwao na
ushindani ulikuwa mkubwa. Tumetolewa kwa penalti tumekubali kushindwa
kwani tulikuwa nyumbani na mpira umechezwa wanastahili pongezi nasi
tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu nyingine zinazofuata," alisema.
0 comments:
Post a Comment