MANCHESTER
United imeonyesha nia ya dhati ya kuipata saini ya nyota wa Aston
Villa, Jack Grealish ili kuongeza nguvu dani ya kikosi hicho kwenye
kipindi cha usajili majira ya joto.
Grealish
ambaye ni nahodha wa Mbwana Samatta amewekwa kwenye hesabu za kutua
United kutokana na kuumia kwa nyota wao Marcus Rashford ambaye atakaa
nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.
Kwenye
Ligi Kuu England, Grealish ametupia mabao saba na pasi tano za mabao
jambo linaloifanya United kumuweka namba moja kwa nyota ambao
wanawaniwa.
Kiungo
huyo mwenye miaka 24 hakuwa na mpango wa kusepa ndani ya mwezi Januari
kwenye klabu hiyo lengo lake lilikuwa ni kuona anatimiza majukumu ndani
ya klabu yake anayoipenda kwa kufanya vizuri kwenye ligi pamoja na Kombe
la Carabao.
Barcelona na Real Madrid nao pia wameongeza uzito kwenye mchakato wa kinasa saini ya nyota huyo.

0 comments:
Post a Comment