Monday, March 16, 2020



DARUWESH Saliboko, Obrey Chirwa, David Molinga na Ayoub Lyanga wametupia mabao nanenane ndani ya Ligi Kuu Bara.

Chirwa ana hat trick mguuni aliwatungua Alliance kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nyamagana wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0.

Saliboko wa Lipuli ana hat trick pia aliwatungua Singida United wakati Lipuli ikishinda kwa mabao 5-1.

Molinga anakimbiza kwa mipira iliyokufa akiwa na mabao matatu ambapo amefunga kwa freekick mbili na penalti moja.

Lyanga mbali na kucheka na nyavu ni mtengeneza nafasi namba moja akiwa ametoa pasi saba za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara.

0 comments:

Post a Comment