Monday, March 16, 2020


Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amewataka wachezaji wachanga wanaochipukia kupewa elimu ya kutosha na muongozo juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
Image result for Wayne Rooney about social
Rooney ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Derby County ni miongoni mwa watumiaji wazuri wa mitandao yao ya kijamii ambapo katika akaunti yake ya Twitter akiwa na wafuatiliaji milioni 17.1, Instragam milioni 14.9 na Facebook milioni 24.
Wayne Rooney says young players need better guidance on how to use their social media platforms
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 amesema kuwa anajuwa uzoefu aliyopitia wakati akiwa na umri wa miaka  18, lakini anasema kwa sasa imekuwa matatizo kwa afya na kuwaaribu saikolojia zao hasa wakati wa mechi.
Rooney ameyasema hayo kupitia Sunday Times, “Changamoto kubwa inayowakumba wachezaji wadogo. Mitandao ya kijamiii ni mizuri kwa namna moja lakini kwa upande mwingine inaweza kuwa mibaya hivyo wanapaswa kufundishwa wachejazi wachanga wanao chipukia namna gani ya kuitumia. Klabu zinapaswa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wachezaji wadogo.”
Dele Alli apologised after posting an offensive video on social media in February
”Hata mimi nilikuwa kwenye umri huo, unatoka kwenye mechi unapitia katika twitter. Kama akaunti yako ya twitter ndiyo ina maelfu ya wafuasi au mamilioni lazima kutakuwa na baadhi ya wachache wakisema mambo mabaya kuhusu nyie.”

0 comments:

Post a Comment