Monday, March 23, 2020


LIGI Kuu ya England huenda ikaanza tena Juni 1 na mechi zote zitachezwa ndani ya wiki sita kukamilisha msimu.
Msimu wa sasa umeahirishwa hadi angalau Aprili 30 kutokana na mlipuko wa virusi vya virusi vya corona Ungereza yote na duniani kwa ujumla. 
Mpango huo utauwezesha msimu mpya wa Ligi Kuu yaq England 2020-2021 kuanza kwa wakati, Agosti 8 - wik nne baada ya kumalizika kwa msimu uliotangulia. 

Ligi Kuu ya England itarejea Juni 1 na kumalizika ndani ya wiki sita 

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, Juni 1, ambayo ni wiki 10 kutoka sasa, si tarehe rasmi bali huo ndio mpango wa Bodi ya Ligi Kuu unaoungwa mkono na Chama cha Soka England .
Kuhakikisha msimu wa sasa unamalizika kutaihakikishia Liverpool taji la kwanza la Ligi Kuu ya England baada ya miaka 30.
Kufuatia Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kuahirisha michuano ya Euro kwa mwaka huu, Bodi imeona Juni 1 itakuwa mwafaka Ligi Kuu ya England kuanza tena.

0 comments:

Post a Comment