Monday, March 23, 2020

Michuano ya Olimpiki
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michuano ya Olimpiki imepengwa kuanza Julai 24, 2020
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inaangalia uwezekano wa kuahirisha michuano ya Tokyo 2020, na imejipatia wiki nne kufanya maamuzi.
Bodi ya Utendaji ya IOC iliyokutana Jumapili jioni huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa wanariadha na kamati za kitaifa za Olimpiki wakitaka michuano hiyo kusogezwa mbele kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
"Kutokana na hali kuwa mbaya duniani kote...bodi ya utendaji leo imeanzisha mchakato mpya wa mpango wa mazingira maalum," taarifa ya IOC imeeleza.
"Mazingira haya maalum yanahusiana na kuboresha mipango iliyokuwepo ya michezo kuanza Julai 24, 2020 lakini pia uwezekano wa kubadili tarehe ya kuanza kwa michezo."
Kuifuta kabisa "si moja ya ajenda" wamesema IOC lakini "kupunguza idadi ya michezo" kunaweza kufikiriwa pia.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amekiri kwa mara ya kwanza kuwa kuwa kuahirisha michuano ya Olimpiki ni jambo linalowezekana endapo hakutakuwa na uwezekano wa kuiandaa kwa "ukamilifu wake".
Woman wearing a mask at a bus stop with Tokyo 2020 advertising
Abe ameliambia bunge la Japani kuwa nchi hiyo inaweza isiwe na "chaguo lengine zaidi ya kuahirisha michuano," huku akisisitiza kuwa kuifuta kabisa michuano hiyo ni jambo lisilowezekana.
Kauli hiyo ya Abe inakuja baada ya mara kadhaa kusema kuwa nchi yake itaweza kuandaa michuano hiyo kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa bila tatizo lolote licha ya mlipuko wa virusi vya corona.
Michuano mbali mbali ya michezo ulimwenguni imesimamishwa kutokana na janga linaloendelea kwa sasa ambapo zaidi ya watu 290,000 wapeta maambukizi ya virusi hivyo huku zaidi ya 12,000 wakipoteza maisha.
Ligi ya Primia (EPL) imeahirishwa mpaka Aprili 4, huku kukiwa na hofu ya muda wa kuahirishwa kuongezwa. Michuano ya Euro 2020 imeahirishwa mpaka 2021.

Canada, Australia kutopeleka wanariadha Tokyo

Canada, Australia kutopeleka wanariadha TokyoWakati IOC na serikali ya Japani wakitazama nini cha kufanya, tayari kamati ya Olimpiki ya Canada imefanya maamuzi ya kutoshiriki michuano hiyo kwa ratiba iliyopo sasa.
Canada inaitaka OIC kuahirisha michuano hiyo kwa mwaka mmoja.
"... kwa sasa dunia ipo katika janga kubwa ambalo ni muhimu kulishughulikia kuliko michezo," imeeleza taarifa ya kamati ya Olimpiki ya Canada.
Kwa upande wa Australia, runinga ya ABC inaripoti kuwa nchi hiyo imewataka wanariadha wake kujiandaa kwa michuano ya Olimpiki kwa mwaka 2021 na si mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment