MSHAMBULIAJI
wa Juventus, Paulo Dybala anakuwa mchezaji wa tatu kugundulika na
Virusi vya Corona ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia,
Serie A.
Nyota huyo mwenye miaka 26 amegundulika na Corona yeye pamoja na mpenzi wake Oriana baada ya kupimwa.
Juventus
imethibitisha kwamba nyota huyo alitengwa tangu Machi 11 ambapo alikuwa
hajaonyesha dalili zozote za ugonjwa mpaka pale kipimo kilipothibitisha
kwamba ameathirika kwani awali aligoma na kukanusha taarifa zilizoelzea
kuwa ana Corona.
Wachezaji wengine ndani ya Juventus ambao wana Corona ni pamoja na Blaise Matuidi na Daniele Rugani.
Mchezaji
wa kwanza ndani ya Serie A kugundulika na Corona alikuwa ni Rugani
ambaye amekuwa akiwapa moyo wachezaji wengine kurejea kwenye morali na
nguvu ya kuamini kwamba wanaweza kupona.
Corona
imekuwa tishio ambapo kwa upande wa michezo ligi zote zimesimamishwa na
zinatarajia kurejea Aprili 30 iwapo hali itakuwa sawa.
0 comments:
Post a Comment