Kutokana
na kutokuwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba,
kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibarahim Ajibu, pamoja na wenzake
wasiokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza, Ijumaa ijayo wanatarajiwa
kupelekwa Simba B.
Kocha
Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amewaandalia wachezaji hao
mechi ya kirafiki na Simba B ambayo watacheza kwa ajili ya kuongeza
viwango vyao katika kipindi hiki ambacho michuano ya Ligi Kuu Bara
imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa.
Sven
alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mikakati yake ya kuhakikisha
wachezaji wote ambao hawana nafasi katika kikosi chake cha kwanza
wanautumia katika kuongeza uwezo wao.
“Licha ya ligi kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, sisi tunaendelea kujifua kama kawaida.
“Tunafanya
mazoezi ya nguvu ambayo yanalenga kabisa kuwaweka sawa wachezaji wote
ili waweze kuwa fiti na zaidi ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi
cha kwanza.
“Kwa
hiyo, siku ya Ijumaa tutakuwa na mechi ya kirafiki na Simba B,
wachezaji ambao watapambana na timu hiyo zaidi watakuwa ni wale ambao
hawana nafasi katika kikosi cha kwanza,” alisema Sven.
0 comments:
Post a Comment