Monday, March 16, 2020



Patrick Cutrone mshambuliaji wa Fiorentina aliyetua hapo kwa mkopo akitokea Wolves amegundulika na virusi vya Corona na kufanya idadi ya waathirika kufikia wanne ndani ya klabu hiyo ya Italia.
Nyota huyo wa Wolves anakipiga kwa mkopo kwenye Klabu ya Fiorentina inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ya Serie A.
Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari kwa mkataba wa muda wa miezi 18 atadumu mpaka mwaka 2021.
Mchezaji mwingine ndani ya Fiorentina ambaye ameathirika na Corona ni German Pezzella baada ya kufanyiwa vipimo.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya Klabu ya Fiorentina imeeleza kuwa "ACF Fiorentina inatangaza kwamba wachezaji wake Patrick Cutrone na German Pezzella na mtaalamu wa masuala ya afya Stefano Dainelli wana Corona ila kwa sasa wanaendelea vizuri pamoja na mshambuliaji Dusan Vlahovic.

0 comments:

Post a Comment