SINGIDA
United inayopambana kujinusuru kushuka Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15
baada ya kucheza mechi 29 nafasi ya 20 imeambulia ushindi wa baada ya
kupitisha dk 1,080 bila kusepa na pointi tatu kwenye mechi zake 12.
Mara ya mwisho Singida United kusepa na pointi tatu ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting Januari 11, iliposhinda bao 1-0.
Baada
ya hapo haikushinda kwenye mechi 12 sawa na dk 1,080, iliambulia sare
mbili kwa kufungana mabao 2-2 na Mwadui, Februari 8 na Alliance 1-1
Singida United, Februari 23 na ilipokea vichapo 10:-Singida United 1-3
Yanga, Januari 22, Kagera Sugar 3-0 Singida United, Februari Mosi,
Biashara United 2-1 Singida United, Februari 5.
Singida
United 0-1 Namungo, Februari 11, Singida United 0-1 Ndanda, Februari
15, Mbao 3-1 Singida United , Februari 18, Singida United 0-1 Polisi
Tanzania, Februari 29, Singida United 0-1 Coastal Union, Machi 4,
Singida United 1-2 Tanzania Prisons, Machi 7, Simba 8-0 Singida United ,
Machi 11.
Imekuja
kuibuka mbele ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Namfua
kwa kuichapa mabao 2-1 juzi Machi 14, huu unakuwa ni ushindi wa tatu kwa
Singida United ambapo wameichapa Mbeya City nje ndani.
0 comments:
Post a Comment