Thursday, April 30, 2020


CRISTIANO Ronaldo nyota anayekipiga
ndani ya Juventus ameombwa na mabosi hao kutotimka kwenye kikosi hicho na adumu mpaka pale mkataba wake utakapomeguka.

Ronaldo mkataba wake ndani ya Juventus unatarajiwa kumeguka 2022 na kwa sasa anatajwa kuwindwa na Real Madrid pamoja na Manchester United ambao wanataka kumrudisha kikosini nyota wao wa zamani.

Kwa sasa Ligi Kuu ya nchini Italia haijaanza na bado Ronaldo hajarejea yupo zake Ureno ambapo alikwenda kumpumzika kutokana na Ligi kusimamishwa baada ya kuibuka janga la Virusi vya Corona.

Juventus ipo nafasi ya kwanza Serie A ikiwa na pointi 63 kibindoni baada ya kucheza mechi 26, imefunga mabao 50 huku Ronaldo akiwa ametupia mabao 21.

0 comments:

Post a Comment