Wednesday, May 27, 2020



UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa umepokea kwa mikono miwili suala la uamuzi wa kutumia Uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Kombe la Shirikisho kwa mikono miwili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa uwanja upo tayari sehemu ya kuchezea na kilichobaki ni kukamilisha sehemu ya jukwaa la mashabiki.

"Tupo vizuri na tumepokea mapendekezo ya kutumia uwanja wa Azam Complex kwa mechi za ligi pamoja na zile za Kombe la Shirikisho, imani yetu ni kwamba kila kitu kitakuwa sawa.

"Tunachosubiri kwa sasa ni kumalizia maboresho ya kwenye sehemu ya kukaa mashabiki ila kwa upande wa sehemu ya kuchezea kila kitu kipo vizuri," amesema.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kurejea Juni Mosi baada ya kusimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

0 comments:

Post a Comment