Jezi
mpya za klabu ya Manchester United za nyumbani zinazodhaniwa kuwa ni za
msimu ujao wa mwaka 2020/21 zimevuja mtandaoni huku mashabiki
wakizisifu kutokana na kuwa na muundo rahisi.
Kulikuwa
na hofu kuwa huwenda jezi hizo zikawa ni zile zilizovuja kabla ya hizi
ambazo mashabiki wengi walizichukia huku muonekano wake wakizifananisha
na siti za basi kupitia akaunti ya mtandao wa Twitter. Lakini mapokezi
ya hizi yamekuwa mazuri zaidi kwa mashabiki.
Jezi iliyowachukiza mashabiki wa United na kulinganishwa na siti za basi
Uzi huo wa Mashetani Wekundu uliovuja kupitia mtandao wa ‘Footy Headlines,’ una rangi nyekundu iliyokolea na logo nyeupe ya Adidas.
0 comments:
Post a Comment