WAKIWA
tayari wana majina ya Michael Sarpong na Jules Ulimwengu wanaocheza
Rwanda, wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM, wamefanya jambo kubwa
lingine kwa kuipa mkataba mashine mpya ya Kinyarwanda ambayo itatua
klabuni hapo msimu ujao.
Mabosi
hao wa GSM wamemalizana na kumpa mkataba beki wa kushoto Erick Rutanga
ambaye kwa misimu miwili Yanga walikuwa wakimfuatilia lakini walishindwa
kumnasa baada ya Rayon Sports kumpa mkataba.
Beki
huyo anakuja kuongeza nguvu kwenye upande wa kushoto wa Yanga ambao kwa
msimu huu unawategemea zaidi Japhary Mohammed na Adeyum Saleh.
Habari
zilizothibitishwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said
ni kuwa beki huyo tayari kila kitu kimeenda sawa na kinachosubiriwa ni
ligi kumalizika kisha beki huyo atue Jangwani.
“Kila
kitu kuhusiana na beki huyo wa kushoto kimeenda sawa na kinachosubiriwa
ni kuja kujiunga na timu kwa msimu ujao baada ya kukubaliana kwenye
mambo ya msingi aliyoyataka.
“Kwa
muda mrefu alikuwa kwenye tageti zetu lakini alisaini mkataba na Rayon
misimu miwili nyuma na sasa anaenda kumaliza mkataba wake kwa hiyo
tulichofanya ni kumuwahi kabisa kwa kukubaliana naye.
“Atakuja
kuungana na wale wengine ambao tumetangaza tayari tumemalizana nao na
wale ambao tuko kwenye mazungumzo ya mwisho kwa ajili ya msimu ujao
kutua kikosini kwetu,” alisema Hersi.
0 comments:
Post a Comment