TIMU
zinazoshiriki Ligi Kuu England kesho zinatarajiwa kupiga kura kuhusu
maamuzi ya kurejea rasmi kwenye mazoezi ya pamoja ili kujiaandaa
kumaliza msimu wa 2019/20.
Kwa
sasa kumekuwa na hofu ya kuanza mazoezi ya pamoja kutokana na janga la
Virusi la Corona ambalo linaivurugavuruga dunia na kufanya shughuli
nyingi zisimamishwe kuepuka maambukizi zaidi.
Mpango
uliopo ni kuona kwamba ligi inarejea Juni ili kumaliza mechi ambazo
zimebaki huku timu zote 20 zikitarajiwa kupiga kura kesho.
Kwa
sasa timu zimeruhusiwa kufanya mazoezi lakini wanafanya kwa
makundimakundi ili kuendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona na
kuna baadhi ya wachezaji ambao wameamua kutojihusisha kabisa na mazoezi
kutokana na hofu waliyonayo.
Timu
nyingi zinaamini kwamba itakuwa ngumu kucheza hivi karibuni kutokana na
wachezaji wao wa kikosi cha kwanza kuwa na hofu ya Corona na wengine
wakiwa wanaumwa jambo ambalo linafanya hofu izidi kutanda.
Baadhi ya nyota ambao wamejiengua kwenye mazoezi ya timu ni pamoja na kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante na Troy Deeney nahodha wa Watford.
0 comments:
Post a Comment