BAADA ya Klabu ya Yanga kudaiwa kuwa
kwenye harakati za chini kwa chini za kumrejesha straika wao wa zamani
raia wa DR Congo, Heritier Makambo, hatimaye dili hilo limetiki baada ya
timu ya Horoya AC kukubali kumuachia nyota huyo.
Makambo
aliachana na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake
kumalizika, kisha akatimkia nchini Guinea ambapo alisajiliwa kwa mkataba
wa miaka mitatu kuitumikia Horoya AC.
Chanzo
chetu makini kimelieleza Championi Jumatano kuwa, baada ya uongozi wa
Yanga kuwa kwenye mazungumzo ya muda wa kuwashawishi mabosi wa Horoya
AC, ili wamrejeshe nyota wao huyo, hatimaye mambo yamekaa sawa baada ya
uongozi huo kukubali kumuachia ajiunge nao kwa miaka miwili.
“Naomba
nikuibie siri tu kwamba, siku si nyingi tunaenda kuwashanganza wale
wote waliokuwa wakidhani hatutaweza kumpata Makambo, eti kutokana na
timu yake kuhitaji dau kubwa kiasi cha wengi kujikuta wakisema Yanga
haitaweza kumrejesha ila kwa taarifa tu ni kwamba muda wowote kuanzia
sasa mambo yataanikwa.
“Wale
ndugu zetu wa Horoya, ni kweli kwamba hawakutaka kabisa kumuachia
Makambo, ila viongozi wenzangu wamepambana vya kutosha kiasi cha
kujikuta wakiwalainisha na kubaki wakituomba watupe kwa mwaka mmoja japo
tumewataka nasi watusikilize zaidi na tayari wameelekea kukubali
kumuachia rasmi ambapo atasaini miaka miwili,” kilisema chanzo
hicho.Makambo amekuwa akitajwa kuwa chaguo namba moja kwenye usajili
ujao wa Yanga na anaaminika kuwa anaweza kufanya mambo makubwa kwenye
timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment